Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhan…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhan…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoing…
Maelezo ya hadith: Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoing…
Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi za mwisho wa ramadhani anauhuisha usiku wote kwa aina mbali mbali za ibada, na anawaamsha familia yake kwa ajili ya swala, na anajitahidi katika ibada zaidi ya kawaida yake, na anajitenga kwa ajili yake na anajitenga na wake zake.
Mafunzo: Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoing…
- Himizo na kufaidika na nyakati bora kwa matendo mema.
- Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Nikuwa inapendeza kuzidisha katika ibada mbali mbali katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na kupendeza kuhuisha siku zake kwa ibada mbali mbali.
- Yampasa kila mja awe na pupa kwa familia yake ya kuwaamrisha kufanya ibada, na awe mvumilivu juu yao.
- Kufanya mambo ya heri kunahitaji uthubutu na subira na kuvumilia.
- Amesema Nawawi: Wametofautiana wanachuoni katika maana ya (Kukaza kikoi) wakasema: Ni kuongeza juhudi katika ibada zaidi ya kawaida yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati zingine, na maana yake: Ni kujipinda katika ibada, husemwa: Jambo hili nimelifungia kikoi, yaani: Nimelidhamiria na nimetenga muda wangu kwa ajili yake, na wamesema wengine: Ni fumbo la kujitenga na wanawake kwa ajili ya kushughulika na ibada.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Funga.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Masiku kumi ya mwisho wa mwezi wa Ramadhani.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur