Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu…

Maelezo ya hadith: Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu…

Ilimfikia habari Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiunganisha swaumu na wala hafungui mwaka mzima, na anaswali usiku mzima wala halali, akamkataza hilo na akamwambia: Funga na ufungue, na simama na ulale. Na akamkataza kuunganisha swaumu na kusimama usiku mzima, na akamwambia: Hakika wewe ukifanya hivyo macho yako yatadhoofika na yatabonyea, na itanyong'onyea kwa hilo nafsi yako na itachoka nakuwa na unyonge; hana swaumu atakayefunga mwaka mzima; kiasi ambacho hakupata malipo ya swaumu kwa kwenda kinyume na katazo, na hakufungua kwa sababu aliendelea. Kisha akamuelekeza kufunga siku tatu katika kila mwezi, hizo ni sawa na swaumu ya mwaka mzima; kwa sababu kila siku moja ni sawa na siku kumi, ambayo ndiyo ziada ndogo zaidi ya mema. Akasema Abdullah: Hakika mimi ninaweza zaidi ya hizo. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Basi funga swaumu ya Daudi amani iwe juu yake na ndiyo swaumu bora, alikuwa akifunga siku moja na anafungua siku moja, na alikuwa hakimbii anapokutana na adui; kwa sababu namna ya swaumu yake haikudhoofisha mwili wake.

Mafunzo: Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Funga. · Fiq'hi na misingi yake. · Funga za Kujikurubisha.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56