Dini ni nasaha

Islam > Sw > Hadith > Daawa na kujitolea kuamrisha mema na kukataza mabaya > Dini ni nasaha

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Dini ni nasaha

عن تميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».

Maelezo ya hadith: Dini ni nasaha

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu, kikamilifu bila uzembe au udanganyifu.

Akaulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nasaha huwa kwa ajili ya nani? Akasema:

Kwanza: Nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha mwingine pamoja naye, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kuzitukuza amri zake, na kulingania watu katika kumuamini.

Pili: Nasaha ni kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu nacho ni Qur'ani Tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, nakuwa kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza, na tunakisoma ukweli wa kukisoma, na tunazifanyia kazi aya zake za wazi, na tunazikubali zenye kutatiza, na tunapinga upotoshaji wa wenye kupindisha, na tunayazingatia mawaidha yake, na kuieneza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo.

Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Tuitakidi kuwa yeye ni Mtume wa mwisho, na tumsadikishe katika yale aliyokuja nayo, na tutekeleze amri zake, na tuyaepuke makatazo yake, na tusimuabudu Allah isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tuitukuze haki yake, na tumuheshimu, na tuutangaze ujumbe wake, na tuisambaze sheria yake, na tuzikanushe tuhuma dhidi yake.

Nne: Nasaha kwa viongozi wa waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu.

Tano: Nasaha kwa waislamu: Kwa kuwafanyia wema na kuwalingania, na kuzuia maudhi dhidi yao, na kuwapendelea kheri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.

Mafunzo: Dini ni nasaha

Makundi : Siasa ya Kisheria. · Haki ya kiongozi kwa Raia. · Da'awa na (kujitolea) kuamrisha mema na kukataza mabaya

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56