Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu r…
Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu r…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zu…
Maelezo ya hadith: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zu…
Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba hajawahi kumuona yeyote nywele za kichwa chake ni ndefu zimefika katika mabega yake, na anayevaa kikoi na shuka jeusi na lenye mistari myekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba miongoni mwa sifa zake za kimaumbile ni kwamba mabega yake yalikuwa mbali mbali, mwenye kifua kipana, na alikuwa na kimo cha kati na kati, kati mrefu na mfupi.
Mafunzo: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zu…
- Hapa kumebainishwa baadhi ya sifa nzuri za Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- katika muonekano, kama uzuri wa nywele na upana wa kifua, na uzuri wa kimo, na mengineyo.
- Mapenzi ya Maswahaba watukufu kwa Mtume- rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba mpaka walikuwa wakielezea na wakiwanukulia waliokuja baada yao miongoni mwa muonekano wake na sifa zake za kimwili na za kimaana (zisizoonekana).
Makundi :
Historia ya Mtume.
· Mambo ya Mtume.
· Sifa za kimaumbile
· Mavazi yake Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake:
· Historia na Taarekh.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله
Gloire à Allah