Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga …

Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga …

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi…

Maelezo ya hadith: Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi…

Lilikuja kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, katika nyumba za wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakiuliza kuhusu ibada zake za siri ndani ya nyumba yake, walipoelezwa wakawa kana kwamba za kwao wameziona ndogo, wakasema: Na tuko wapi sisi na Mtume rehema na amani ziwe juu yake? hali yakuwa amekwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, ukilinganisha na ambaye hajajua hata kupatikana kwa msamaha, huyu anahitaji kupitiliza katika kufanya ibada huenda akaupata msamaha huo. Kisha wakasema baadhi yao: Sitooa wanawake. Na wakasema baadhi yao: Sitokula nyama. Na wakasema baadhi yao: Sitolala katika godoro. Hilo likamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akachukia, na akawahutubia watu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamtukuza, na akasema: Wana nini watu fulani waliosema kadhaa wa kadhaa?! Wallahi mimi ndiye ninayemuhofu sana Mwenyezi Mungu kuliko watu wote na ndiyo mchamungu wenu, lakini ninalala ili nipate nguvu ya kusimama, na ninafungua ili nipate nguvu ya kufunga, na ninaoa wanawake, atakayeipuuza njia yangu, na akaona njia nyingine ndio iliyokamilika, na akachukua njia ya asiyekuwa mimi, huyu hayuko nami.

Mafunzo: Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi…

Makundi : Historia ya Mtume. · Mambo ya Mtume. · Muongozo wa Mtume. · Historia na Taarekh.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56