Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema:…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema:…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swa…

عن عَبْد اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قال: «أّعْتَمَ النَبِيُّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِالعِشَاء، فَخَرَج عُمَر فقال: الصَّلاةَ يا رسول الله، رَقَد النِسَاءُ والصِّبيَان. فَخَرَجَ ورَأسُهُ يَقطُر يقول: لَولاَ أن أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي -أو على النَّاس- لَأَمَرتُهُم بهذه الصَّلاة هذه السَّاعَة».

Maelezo ya hadith: Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swa…

Alichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Historia ya Mtume. · Fiq'hi na misingi yake. · Mambo ya Mtume. · Masharti ya Swala. · Sifa za kitabia. · Huruma yake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: · Historia na Taarekh.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
حسبنا الله ونعم الوكيل Allah nous suffit, quel excellent protecteur

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56