Islam > Sw > Hadith > Historia ya mtume > Ya kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kwenda kw…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAnaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake, ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kabla ya kifo chake kwa Wafalme wa mataifa waliopembezoni mwake, akiwaita katika Uislamu; akamuandikia Kisra, nalo ni jina la kupachikwa la kila Mfalme Uajemi, na kwenda kwa Kaisari, nalo ni jina la kupachikwa kwa kila mfalme wa Roma, na kwenda kwa Najashi nalo ni jina la kupachikwa la kila mfalme wa uhabeshi. Na akaandika pia kwenda kwa kila mfalme jeuri mwenye kuwakandamiza watu, na mwenye kuwatenza nguvu, na akabainisha Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Najashi aliyetumiwa Ujumbe si Najashi yule aliyesilimu na akafariki na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamswali swala ya maiti asiyekuwepo.
Makundi : Historia ya Mtume. · Mikataba yake na jumbe zake Mtume rehema na Amani za Allah ziwe juu yake: · Historia na Taarekh.