Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani lim…
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani lim…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake…
Maelezo ya hadith: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake…
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.
Mafunzo: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake…
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama vile kuipa nyongo dunia na kuzipuuza ladha za dunia, pamnoja nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa uwezo wa hilo lau kama angetaka kustarehe nayo.
- Inafaa kutumia magodoro na mito, na kuvilalia na kuwa juu yake.
- Muislamu anatakiwa kuzingatia hali yake na hali ya maisha ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake. Kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba mwenye kuiga nyenendo zake ataongoka na atafaulu duniani na Akhera.
- Kuwa na pupa ya kuiandaa Akhera, na muumini atosheke katika dunia na kile kinachomsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, na asishughulike na kutafuta wingi wa mali ndani yake, na aliwakemea Mwenyezi Mungu watu, akasema: "Kumekupumbazeni kutafuta wingi (wa mali) mpaka mkayazuru makaburi" [Takathur: 1-2].
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.
· Historia ya Mtume.
· Mambo ya Mtume.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Muongozo wa Mtume.
· Historia na Taarekh.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah