Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na…
Maelezo ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu anapenda kwa waja wake mambo matatu, na anachukia kutoka kwao mambo matatu, anapenda kutoka kwao: Wampwekeshe yeye pekee na wala wasimshirikishe na chochote, na washikamane na ahadi ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na mafundisho ya Nabii wake wote, na wala wasifarakane katika umoja wa Waislamu. Na anachukia kwao: Upuuzi na maneno yasiyokuwa na faida katika yale yasiyowahusu, na kuuliza jambo ambalo bado halijatokea, au kuwaomba watu mali zao, na vile wanavyovimiliki, na yale yasiyokuwa na ulazima wa kuyaomba, na kupoteza mali na kuzitumia katika njia zisizokuwa za kisheria, na kuziweka katika uharibifu.
Mafunzo: Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na…
- Anapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa waja wake utakasifu katika ibada zake, na anachukia kumkufuru.
- Himizo la kushikana katika kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa ndani yake kuna umoja na maelewano.
- Himizo la umoja, na amri ya kushikamana nao na kuziweka pamoja safu zake, na katazo la kinyume chake kama kufarakana na kuhitilafiana.
- Katazo la kukithirisha maneno kwa yale yasiyomuhusu; kwa sababu yakiwa ni ya halali basi ndani yake kuna kupoteza wakati, na yakiwa ya haramu basi kutakuwa na madhambi mengi.
- Katazo la kujiingiza katika habari za watu na kufuatilia hali zao na kusimulia kauli zao na matendo yao.
- Katazo la kukithirisha maswali katika mambo ya watu.
- Uharamu wa kupoteza mali, na himizo la kuzihifadhi na kuzitumia katika yale yanayofaa.
Makundi :
Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia.
· Jamii ya Kiislamu
· Akida- Itikadi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah