Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na …
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu…
Maelezo ya hadith: Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji.
Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.
Mafunzo: Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu…
- Hili ni himizo kwa waislamu kusaidizana katika heri.
- Amesema bin Hajar: Katika Hadithi hii kuna himizo la kuwafanyia wema wale wanaowafanyia wema Waislamu, au kutekeleza moja ya wajibu wao.
- Kanuni ya jumla nikuwa: Yeyote anayemsaidia mtu katika kumtii Mwenyezi Mungu atapata malipo sawa na malipo yake, bila ya kupunguzwa ujira wake hata kidogo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Jihadi.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Fadhila za Jihadi.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah