Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko sik…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko sik…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Bukhari na Abu Daud na matamshi ya hadithi ni yake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani…

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «ما مِنْ أيَّامٍ العمَلُ الصَّالِحُ فيها أحبُّ إلى اللهِ مِن هذه الأيام» يعني أيامَ العشر، قالوا: يا رسُولَ الله، ولا الجهادُ في سبيلِ الله؟ قال: «ولا الجهادُ في سبيلِ الله، إلا رجلٌ خَرَجَ بنفسِه ومالِه فلم يَرْجِعْ من ذلك بشيءٍ».

Maelezo ya hadith: Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani…

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa amali njema ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi Dhul-Hija ni bora kuliko siku zingine.

Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kupigana Jihadi katika siku kumi hizi, je ni bora au kufanya matendo mema katika siku hizi? Kwakuwa linajulikana kwao kuwa Jihadi ni amali bora.

Akajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Yakuwa amali njema ndani ya siku hizi ni bora kuliko Jihadi katika siku zingine, isipokuwa mtu aliyetoka Jihadi na akaihatarisha nafsi yake na mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, akapoteza mali yake na ikatoka roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hiki ndicho kilicho bora kuliko amali njema ndani ya siku hizi bora.

Mafunzo: Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Hijja na Umra. · Jihadi. · Fiq'hi na misingi yake. · Masiku kumi ya Dhul hijjah. · Fadhila za Jihadi.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56