Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu,…

Islam > Sw > Hadith > Uzushi > Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (vijana), wenye mawazo ya kipumbavu,…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (…

Maelezo ya hadith: Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (…

Ameeleza kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba, mtakaponisikia ninakuhadithieni kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi hakika mimi sifichi wala sibuni, wala sifuniki haki, bali ninaweka wazi, na kuanguka kwangu kutoka juu mbinguni ni rahisi na ni bora sana kwangu kuliko kusimulia jambo la uongo nikasema kuwa limetoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na nikisimulia mambo yalio kati yangu mimi na watu wengine, basi vita ni udanganyifu, hapo ninaweza kusema kwa mafumbo au kubuni au kuficha, kwani nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Watatokea katika zama za mwisho vijana wenye umri mdogo, wasiojitambua (madhaifu wa akili) watakuwa wakisema maneno kutoka ndani ya Qur'ani na wakiisoma kwa wingi, watakuwa wakitoka ndani ya Uislamu na wakivuka mipaka yake, kama mshale utokavyo katika upinde, Imani yao haivuki koromeo zao, mahali popote mtakapokutana nao basi wauweni, kwani kuwaua kwao kuna malipo kwa atakayewauwa, siku ya Kiyama.

Mafunzo: Watatokea katika zama za mwisho watu wenye umri mdogo (…

Makundi : Uzushi. · Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Jihadi. · Akida- Itikadi- · Fiq'hi na misingi yake. · Ahl-us-Sunnah's (Sunni) Stance on Religious Innovators · Rulings of Terrorism, Assassinations, and Explosions · Kuamini mitume · Majina na Hukumu. · Karama za Mawalii.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56