Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
Maelezo ya hadith: Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa peponi kuna daraja na vituo mia moja, na masafa yaliyopo kati ya daraja mbili ni kama masafa kati ya mbingu na ardhi, na Pepo ya juu zaidi miogongoni mwa Pepo hizi ni Pepo ya Firdausi, na ndani yake ndiko inapochimbuka mito yote minne ya Pepo, na juu ya Firdausi ndiko inakokuwa Arshi; mkimuomba Mwenyezi Mungu basi muombeni Firdausi; kwani ndiyo iko juu ya Pepo zote.
Mafunzo: Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
- Kutofautiana kwa vituo vya watu wa Peponi, na hii ni kulingana na imani na mtendo mema.
- Himizo la kumuomba Mwenyezi Mungu Firdausi ya juu katika Pepo.
- Firdausi ndiyo Pepo ya juu, na ndio bora zaidi kuliko zote.
- Ni wajibu kwa muislamu hamu yake kuwa ya juu zaidi, na aende mbio na aombe makazi ya juu na bora zaidi kuliko yote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Mito minne ya Pepo ni mito ya maji na maziwa na mvinyo na asali iliyotajwa ndani ya Qur'ani katika kauli yake Mtukufu: "Mfano wa Pepo waliyoahidiwa wachamungu, ndani yake kuna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa" [Muhammadi: 15].
Makundi :
Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali.
· Akida- Itikadi-
· Dua zilizopokelewa toka kwa mtume.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Kuamini siku ya mwisho
· Maisha ya Akhera.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur