Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
عن أبي مَرْثَدٍ الغَنَوِيّ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ، وَلَا تُصَلُّوا إِلَيْهَا».
Maelezo ya hadith: Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi.
Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.
Mafunzo: Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
- Katazo la kusali makaburini au kati kati yake au kuyaelekea, isipokuwa swala ya jeneza kama ilivyothibiti katika mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
- Katazo la kusali kwa kuyaelekea makaburi ni kuziba mianya ya kuingia katika ushirikina.
- Uislamu umekataa kuchupa mipaka katika makaburi na kuyadhalilisha pia, hakuna kuyapuuza wala kuyatukuza.
- Heshima ya muislamu inabakia hata baada ya kufa kwake, kwa kauli yake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai".
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Sala.
· Akida- Itikadi-
· Fiq'hi na misingi yake.
· Masharti ya Swala.
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad