Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii w…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii w…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara…

عن عائشة أم المؤمنين وعبد الله بن عباس رضي الله عنهما قالا: لَمَّا نَزَلَ بِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَفِقَ يَطْرَحُ خَمِيصَةً لَهُ عَلَى وَجْهِهِ، فَإِذَا اغْتَمَّ بِهَا كَشَفَهَا عَنْ وَجْهِهِ، فَقَالَ وَهُوَ كَذَلِكَ: «لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى اليَهُودِ وَالنَّصَارَى، اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ» يُحَذِّرُ مَا صَنَعُوا.

Maelezo ya hadith: Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara…

Anaeleza Aisha na bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakuwa kilimpofika kifo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alianza kuweka kipande cha kitambaa juu ya uso wake, akibanwa na pumzi kwa sababu ya kilevi cha kifo anakitoa usoni kwake, akasema akiwa katika hali hiyo mbaya: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Manaswara, na akawafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao walijenga Misikiti juu ya makaburi ya Manabii wao, laiti kama jambo hili lisingekuwa na hatari basi asingelieleza katika sehemu kama hii, kwa sababu hii ameukataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kufanana na kitendo hicho; kwa sababu ni katika vitendo vya Mayahudi na Manaswara, na ni kwa sababu ni njia inayopelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo: Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56