Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, n…

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, n…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineo

Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu…

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لِي عَنْ أُمَّتِي الخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ».

Maelezo ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu…

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wake katika hali tatu: La kwanza: Kukosea, nayo ni yale yanayotokea kwao pasina kukusudia, nayo ni muislamu kukusudia kufanya jambo lolote, kisha kitendo chake kikakutana na jambo ambalo hakulikusudia. La pili: Kusahau, nako ni muislamu kuwa na kumbukumbu ya kitu, lakini akakisahau wakati wa kufanya, hana madhambi katika hilo pia. La tatu: Kulazimishwa, mja anaweza kulazimishwa kufanya kitu ambacho hakitaki pamoja na kutoweza kuzuia kulazimishwa, na hapo pia hatopata dhambi au ubaya. Pamoja na tahadhari kuwa maudhui ya hadithi ni katika yale yalio baina ya mja na Mola wake katika kufanya maharamisho, ama kuacha maamrisho kwa kusahau hapa haiondoki, na ama kitendo chake kikiambatana na kosa la jinai hii pia haiondoki katika haki ya kiumbe, kama akiua kimakosa, atatakiwa kutoa fidia, au akaharibu gari kwa makosa atawajibika kulipa.

Mafunzo: Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu…

Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.7 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56