Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi y…
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi y…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Nasai katika Sunan Alkubra na Ibn Majah na Ahmad
Upokezi wake ni mzuri
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zi…
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما: أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَلَّمَهُ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ، فَقَالَ: مَا شَاءَ اللهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ عَدْلًا؟ قُلْ: مَا شَاءَ اللهُ وَحْدَهُ».
Maelezo ya hadith: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zi…
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.
Mafunzo: Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zi…
- Katazo la kusema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka, na mfano wake katika yale yanayounganisha matashi ya mja katika matashi ya Mwenyezi Mungu kwa "na"; kwani hii ni katika shirki ndogo.
- Ulazima wa kukemea uovu.
- Mtume rehema na amani zimfikie alilinda mipaka ya tauhidi, na akaziba njia za ushirikina.
- Wakati wa kuondoa uovu ni vyema kumuelekeza anayefikishiwa ujumbe katika mbadala wa halali, kwa kumuiga Mtume rehema na amani zimfikie.
- Kukusanya baina ya kauli yake rehema na amani zimfikie katika hadithi hii: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", na kauli yake katika hadithi nyingine: "Sema: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe" Nikuwa kauli ya mtu: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe", hii inafaa, lakini kauli ya: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake" ndio bora zaidi.
- Inafaa kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka" lakini bora zaidi ni kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka
· Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah