Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake m…

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hivi" Kisha akapiga kwa mikono yake m…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hi…

عَنْ عَمَّارِ بنِ ياسِرٍ رضي الله عنه قال: بَعَثَنِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَاجَةٍ، فَأَجْنَبْتُ فَلَمْ أَجِدِ الْمَاءَ، فَتَمَرَّغْتُ فِي الصَّعِيدِ كَمَا تَمَرَّغُ الدَّابَّةُ ثُمَّ أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لَهُ فَقَالَ: «إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَقُولَ بِيَدَيْكَ هَكَذَا» ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدَيْهِ الْأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً، ثُمَّ مَسَحَ الشِّمَالَ عَلَى الْيَمِينِ، وَظَاهِرَ كَفَّيْهِ وَوَجْهَهُ.

Maelezo ya hadith: Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hi…

Alimtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ammari Bin Yasiri radhi za Allah ziwe juu yake katika moja ya safari kwa baadhi ya haja zake, akapatwa na janaba kwa tendo la ndoa au kushukwa na manii kwa matamanio, na hakupata maji ili aoge, Na alikuwa hajui hukumu ya tayamam kwa ajili ya janaba, bali alikuwa anajua hukumu yake kwa hadathi ndogo, akajitahidi na akadhani kuwa kama ambavyo hufuta kwa udongo baadhi ya viungo vya udhu kwa kuondoa hadathi ndogo, akaona kuwa kutayamam kwa kuondoa janaba ni lazima aeneze udongo mwili mzima; kwa kuchukulia kipimo katika maji, akajigeuzageuza katika udogo mpaka akaueneza mwili mzima na akaswali, alipokuja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamueleza kuhusu hilo; ili aone je yeye amepatia au amekosea? Akambainishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- namna ya kujitwaharisha kutokana na hadathi mbili, ndogo kama haja ndogo, na hadathi kubwa kama janaba: Nako ni mtu kupiga kwa mikono yake miwili juu ya udongo mpigo mmoja, kisha afute kwa mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake.

Mafunzo: Hakika ilikuwa inakutosheleza kupiga kwa mikono yako hi…

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Twahara - usafi- · Fiq'hi na misingi yake. · Kutayammam

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56