Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafs…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafs…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na k…

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «الْكَبَائِرُ: الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ، وَقَتْلُ النَّفْسِ، وَالْيَمِينُ الْغَمُوسُ».

Maelezo ya hadith: Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na k…

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- madhambi makubwa, nayo ni yale aliyokemewa mfanyaji wake kwa kemeo la adhabu kali duniani au Akhera.

La kwanza lake "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu": Nalo ni kukielekeza chochote katika aina za ibada kwa asiyekuwa Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika yale ambayo ni maalumu kwa Allah katika uungu wake na uumbaji wake na majina yake na sifa zake.

Na la pili lake "Ni kuwaasi wazazi wawili": Nalo ni kila linalopelekea kuwaudhi wazazi wawili sawa sawa iwe kauli au kitendo, na kuacha kuwatendea wema.

Na la tatu lake: "Ni kuua nafsi": Bila hatia, kama kuuwa kwa dhulma na uadui.

Na la nne lake "Kiapo cha uongo": Nako ni kuapia uongo huku ukijua kuwa ni uongo, umeitwa hivyo; Kwa sababu humzamisha mfanyaji wake katika madhambi au motoni.

Mafunzo: Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na k…

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Kuyasema vibaya Maasi. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.7 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56