Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo …
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo …
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyek…
Maelezo ya hadith: Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyek…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.
Mafunzo: Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyek…
- Kutosheka ni miongoni mwa tabia tukufu za muumini, nayo ni katika alama za kuridhia makadirio ya Mwenyezi Mungu.
- Amesema bin Jariri: Hii ni hadithi iliyokusanya aina nyingi za kheri; kwa sababu mtu anapoona mtu aliyefadhilishwa katika dunia basi hutamani apate mfano wake, na kuyadogesha aliyonayo katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anapata tamaa ya kuongeza ili amfikie huyo au amkaribie, hili ndilo liliopo kwa watu wengi, na ama akimtazama katika mambo ya kidunia yule aliye chini yake katika yale yaliyodhihiri kwake katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu anazomzidi, akamshukuru na akanyenyekea, na akafanya kheri ndani yake.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuzitakasa Nafsi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah