Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, la…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, la…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Albayhaqy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wang…
عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال: «لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، ولَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».
Maelezo ya hadith: Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wang…
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.
Mafunzo: Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wang…
- Amesema bin Daqiq Al-Idd: Na hadithi hii ni msingi katika misingi ya utoaji wa hukumu, na ni marejeo makubwa wakati wa mzozo na ugomvi.
- Sheria imekuja kulinda mali za watu na damu zao zisichezewe.
- Hakimu asikuhumu kwa elimu yake bali arudi katika ushahidi.
- Yeyote atakayedai madai ambayo hayana uthibitisho yatakataliwa, iwe yanahusu haki na miamala au masuala ya imani na sayansi.
Makundi :
kuhukumu.
· Madai na Ushahidi.
· Fiq'hi na misingi yake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur