Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katik…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureAmeeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hatovuka mtu yeyote kisimamo cha hesabu siku ya Kiyama kwenda peponi au motoni mpaka aulizwe kuhusu mambo kadhaa:
La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini?
La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki?
La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?.
La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?
Makundi : Akida- Itikadi- · Kuamini siku ya mwisho · Maisha ya Akhera.