Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi hus…
Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi hus…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo z…
Maelezo ya hadith: Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo z…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.
Mafunzo: Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo z…
- Maiti mwema huanza kuona habari njema kabla ya kuzikwa kwake, na kafiri hufadhaika, na kuona mambo kinyume na hivyo.
- Baadhi ya suti husikiwa na viumbe vingine tofauti na mwanadamu, na wala mwanadamu hawezi kuzisikia.
- Sunna ni kulibeba Jeneza juu ya mabeba ya wanaume na si wanawake; kwa katazo la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwakataza wanawake kusindikiza Jeneza.
Makundi :
Akida- Itikadi-
· Kuamini siku ya mwisho
· Maisha ya Barzakhi (Baada ya kufa)
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الله أكبر
Allah est le plus grand