Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu wa ibada mbalimbali > Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Maelezo ya hadith: Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Anatuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Tuseme na turudie neno la kumpwekesha "Laa ilaah illa llaah" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kufikwa kwake na tabu za kifo mpaka aliseme, ili liwe neno lake la mwisho.
Mafunzo: Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
- Sunna ya kumtamkisha aliyefikwa na mauti.
- Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
- Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
- Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
- Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Majeneza.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Mauti na Hukumu zake.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah