Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utaku…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureMikidadi bin Aswadi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi atakapokutana na mtu miongoni mwa makafiri katika mapambano, wakapambana kwa mapanga, mpaka yule kafiri akakata mmoja kati ya mikono yake kwa upanga, kisha kafiri akamkimbia na akajikinga katika mti, akasema: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, je, ni halali kwangu kumuua baada yakuwa amekata mkono wangu?
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Hapana, usimuuwe.
Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lakini yeye kakata moja ya mikono yangu, pamoja na hivyo bado tu nisimuuwe?!
Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hapana, usimuuwe, kwa sababu tayari damu yake ishakuwa haramu, kwa sababu ikiwa utamuua baada ya kusilimu kwake; basi hakika yeye atakuwa katika nafasi yako ya kulindwa damu kwa Uislamu wake, na wewe utakuwa katika nafasi yake, itakuwa halali damu yako kwa kukuua kwa kisasi kwa sababu ya kumuuwa.
Makundi : Akida- Itikadi- · Majina na Hukumu. · Uislamu