Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachu…
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachu…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa ka…
Maelezo ya hadith: Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa ka…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.
Mafunzo: Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa ka…
- Fadhila za kuvumilia balaa, na kuacha kuchukia na kulalamikia maumivu, ili hilo lisipelekee katika jambo baya zaidi kuliko hilo.
- Kuhadithia kuhusu Umma zilizopita kwa yale ambayo yana kheri na mawaidha ndani yake.
- Amesema bin Hajari: Hapa kuna kusimama katika haki za Mwenyezi Mungu na rehema zake na kwa viumbe wake, kiasi ambacho amewaharamishia kujiua, na kwamba nafsi ni milki ya Mwenyezi Mungu.
- Uharamu wa kutumia sababu zinazopelekea katika kuia nafsi, na onyo kali katika hilo.
- Amesema bin Hajari: Na imeonyesha kuwa alijikata kwa ajili ya kujiua na si kwa kutaka kujitibu, ambayo inaweza kuwa dhana ya kunufaika na kitendo hicho.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuyasema vibaya Maasi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah