Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi
عَنْ المُغِيرَةِ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: «دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ» فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا.
Maelezo ya hadith: Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.
Mafunzo: Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi
- Sheria ya kufuta juu ya khufu mbili inakuwa wakati wa kutia udhu kwa ajili ya hadathi ndogo, ama kuoga kwa ajili ya hadathi kubwa ni lazima kuosha miguu.
- Kufuta kunakuwa mara moja kwa kupitisha mkono ulioloana juu ya khufu nasi chini yake.
- Ni sharti wakati wa kufuta juu ya khufu iwe kuzivaa kwake ni baada ya udhu kamili ambao aliosha miguu yake wakati huo kwa maji, na khufu ziwe twahara (safi) na zifunike mahali panapolazimika kuoshwa katika miguu, na kuwe kufuta ni katika hadathi ndogo si katika janaba au chochote kinachowajibisha kuoga, na kufuta kuwe katika muda uliopangwa kisheria nao ni usiku na mchana kwa mwenyeji na siku tatu kwa msafiri.
- Kitapimwa katika khufu mbili kila chenye kusitiri miguu miwili kama soksi na kinginecho, inafaa kufuta juu yake.
- Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mafundisho yake, kiasi kwamba alimzuia Mughira kumvua, na akamueleza sababu: Kuwa alizivaa akiwa twahara; ili nafsi yake itulizane, na ajue hukumu ya hilo.
Makundi :
Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali.
· Twahara - usafi-
· Adabu za kisheria.
· Adabu na Hukumu za Safari.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا إله إلا الله
Pas de divinité sauf Allah