Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo …

Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo …

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujivi…

Maelezo ya hadith: Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujivi…

Aliambiwa Osama bin Zaid Mwenyezi Mungu awawie radhi wote wawili: Hivi huendi kwa Othman bin Affan, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ukamwambia kuhusu fitina zilizotokea baina ya watu na kutafuta kuzizima. Basi akawaeleza kuwa alizungumza naye kwa siri ili kutafuta maslahi, si kuchochea kwa fitina, na lengo lake lilikuwa kwamba hataki kuwashutumu viongozi hadharani, ikawa ni sababu ya kurefusha mzozo kwa kiongozi, na ni mlango wa fitina na uovu, na siwezi kuwa wa kwanza kuufungua.

Kisha Osama Mwenyezi Mungu awawie radhi, akasema kuwa: Anawanasihi viongozi kwa siri na wala hambembelezi yeyote kwa kumsifu, hata akiwa kiongozi, na wala hawabembelezi kwa kuwasifu kwa uongo, na hiyo ni baada ya yeye kuwa alisikia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ataletwa mtu Siku ya Kiyama na kutupwa Motoni, na utumbo wake utatoka nje ya tumbo lake kutokana na ukali wa adhabu, na atasokota utumbo wake katika hali hii Motoni kama punda anayezunguka jiwe lake la kusagia nafaka, watu wa Motoni watamzunguka kwa duara kisha watamuuliza: Ewe fulani, je si wewe aliyekuwa ukiamrisha mema na kukataza maovu?!

Atasema: Mimi nilikuwa nikiamrisha mema na wala siyafanyi, na ninakataza maovu na ninayafanya.

Mafunzo: Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujivi…

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Sifa za pepo na moto. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56