Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, …

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, …

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ibn Abii Shaybah

Ni sahihi kwa njia zake na ushahidi wake

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu…

عن علي بن الحسين: "أنه رأى رجلا يجيء إلى فُرْجَةٍ كانت عند قبر النبي صلى الله عليه وسلم فيدخل فيها فيدعو، فنهاه، وقال: ألا أحدثكم حديثا سمعته من أبي عن جدي عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:« لا تتخذوا قبري عيدا، ولا بيوتكم قبورا، وصلوا علي، فإن تسليمكم يبلغني أين كنتم».

Maelezo ya hadith: Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu…

Anatueleza Ally bin Husein -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuona mtu mmoja akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, nakuwa yeye alimkataza juu ya hilo kwa ushahidi wa hadithi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ambayo limekuja ndani yake katazo la kulifanyia mazoea kaburi lake kwa ziara, na katazo la kuzitelekeza nyumba kwa kutokuwa na ibada ya Mwenyezi Mungu ndani yake na dhikri, na kuifananisha kwake na kaburi, na akaeleza kuwa salamu ya muislamu itamfikia yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- mahala popote atakapokuwa muislamu.

Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Tauhiid. · Fiq'hi na misingi yake. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima. · Hukumu za Misikiti.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا حول ولا قوة إلا بالله Pas de force ni de puissance sauf en Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56