Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamj…
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamj…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy, Ahmad na Ad-Darimi
Ni nzuri (Hasan)
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu ya…
Maelezo ya hadith: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu ya…
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Assalaam alaikum" Akamjibu kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ameandikiwa mema kumi, kisha akaja mtu mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi" Akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Amepata thawabu ishirini, kisha akaja mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", akamjibu akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kapata thawabu thelathini; yaani kwa kila tamko ni mema kumi.
Mafunzo: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu ya…
- Anayefika awaanze waliokaa kwa salamu.
- Malipo kuongezeka kwa kuzidi matamshi ya salamu.
- Ukamilifu katika kutoa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na namna nzuri katika kujibu: Ni "Waalaikumus salaam warahmatullaahi wabarakaatuh".
- Daraja za kutoa salamu na kujibu zinatofautiana, vile vile malipo yanatofautiana.
- Kuwafundisha watu kheri na kuwatanabahisha ili kufanya lililobora zaidi.
- Amesema bin Hajari: Ikiwa atazidisha mwenye kuanza "Warahmatullah" basi ni sunna kwake "wabarakaatuh", na ikiwa atazidisha "wabarakaatuh" je ni sheria pia kuzidisha wakati wa kujibu? Na vile vile ikiwa atazidisha mwenye kuanza "wabarakaatuh" je ni sheria kwake kufanya hivyo, ameitoa Maliki katika Muwattwa'a kutoka kwa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Salamu imeishia katika baraka.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za kutoa salamu na kubisha Hodi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur