Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mun…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mun…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia pepo…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ أَعْرَابِيًّا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ دَخَلْتُ الجَنَّةَ، قَالَ: «تَعْبُدُ اللَّهَ لاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا، وَتُقِيمُ الصَّلاَةَ المَكْتُوبَةَ، وَتُؤَدِّي الزَّكَاةَ المَفْرُوضَةَ، وَتَصُومُ رَمَضَانَ» قَالَ: وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ أَزِيدُ عَلَى هَذَا، فَلَمَّا وَلَّى قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى رَجُلٍ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، فَلْيَنْظُرْ إِلَى هَذَا».

Maelezo ya hadith: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia pepo…

Alikuja mtu mmoja miongoni mwa watu wa vijijini kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amjulishe kuhusu amali itakayomuingiza peponi, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kuwa kuingia peponi na kuokoka na moto yote haya yanasimama katika nguzo za Uislamu, kuanzia kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na usimshirikishe na kitu chochote katika ibada. Na usimamishe swala tano alizoziwajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika kila usiku na mchana. Na utoe zaka ya mali aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu juu yako, na uitoe kuwapa wastahiki wake. Na uhifadhi na kudumu nayo swaumu ya ramadhani katika wakati wake. Yule bwana akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha chochote zaidi ya amali hizo za faradhi nilizozisikia toka kwako katika ibada, na wala sitopunza chochote katika hizo. Alipoondoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Yeyote atakayependezwa na kumuangalia mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame bedui (Mtu wa kijijini) huyu.

Mafunzo: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia pepo…

Makundi : Adabu za kisheria. · Adabu za mjuzi na mwenye kujifunza. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56