Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, …
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ، وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ، وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ، وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ».
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu.
Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru.
Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika.
Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo.
Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).
Makundi : Adabu za kisheria. · Adabu za kutoa salamu na kubisha Hodi. · Adabu za kupiga Chafya na Miayo. · Adabu za kumtembelea mgonjwa. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.