Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza w…
Maelezo ya hadith: Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza w…
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu mtenda dhambi anatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa mwenye kutangaza maasi kwa kutaka ufahari na jeuri, huyu hastahiki msamaha; anafanya maasi mchana, kisha anaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, anaanza kumsimulia mwingine kuwa yeye jana alifanya maasi fulani, na hali yakuwa alilala Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka anafunua pazia la Mwenyezi Mungu juu yake!!.
Mafunzo: Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza w…
- Ubaya wa kuweka wazi maasi baada ya kusitiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Katika kutangaza maasi ni kusambaza machafu baina ya waumini.
- Mwenye kusitiriwa na Mwenyezi Mungu duniani atamsitiri pia Akhera, na hii ni katika upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.
- Atakayepata mtihani wa maasi, anatakiwa ajifiche, na atubie kwa Mwenyezi Mungu.
- Ukubwa wa dhambi la kutangaza madhambi kwa wale wanaokusudia kuweka wazi maasi, na wanajikosesha wao wenyewe kusamehewa.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuyasema vibaya Maasi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad