Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfa…

Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni mwa uongofu na elimu ni sawa na mfa…

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni…

Maelezo ya hadith: Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni…

Amefananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kumstaajabu yule anayenufaika na yale aliyokuja nayo miongoni mwa muongozo na njia inayomfikisha mtu katika lengo, na elimu ya kisheria na Ardhi ambayo inashukiwa na mvua nyingi; ikawa migawanyiko mitatu: Wa kwanza: Ardhi safi nzuri, inayokubali maji ya mvua, ikaotesha mimea mingi mibichi na mikavu, watu wakanufanika nayo. Wa pili: Ardhi inayotunza maji lakini haioteshi mimea, yenyewe inahifadhi maji ili watu wanufaike nayo; wanakunywa na kunywesha mifugo yao na mazao yao. Wa tatu: Ni Ardhi tambarare kavu haitunzi maji na wala haioteshi mazao, yenyewe haikunufaika na maji hayo, na wala watu hawakunufaika nayo. Ndivyo hivyo wenye kusikiliza yale aliyotumwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa elimu na uongofu. Wa kwanza: Ni mwanachuoni mwenye utambuzi katika dini, mwenye kuifanyia kazi elimu yake, mwenye kumfundisha mwingine; huyu yuko katika nafasi ya Ardhi nzuri, iliyokunywa ikanufaika yenyewe na ikaotesha ikamnufaisha mwingine. Wa pili: Ni yule aliyehifadhi elimu lakini hana uelewa na namna ya kuitumia, huyu kakusanya elimu, na amemaliza muda wake wote kwa hilo, isipokuwa yeye hajafanyia kazi sunna zake, na wala hana uelewa wa yale aliyoyakusanya; yeye ni mfano wa chombo kwa wengine, na yeye ni sawa na Ardhi ambayo maji hutuama ndani yake na watu wakanufaika nayo. Wa tatu: Ni yule anayesikia elimu lakini haihifadhi, na wala haifanyii kazi, na wala hainukuu kumpa mwingine; huyu ni kama Ardhi kavu ngumu isiyokuwa na mimea ndani yake, wala haikubali maji au inayomharibia mwingine.

Mafunzo: Mfano wa yale aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu miongoni…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Elimu. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
الحمد لله Louange à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56