Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَنْكِبِي، فَقَالَ: «كُنْ فِي الدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ»، وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ، يَقُولُ: إِذَا أَمْسَيْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ الصَّبَاحَ، وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ المَسَاءَ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ، وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ.

Maelezo ya hadith: Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia

Ibn Omari Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ameeleza kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika begani - nacho ni kiungo cha juu cha mkono na bega - akamwambia: Kuwa katika dunia hii kana kwamba wewe ni mgeni aliyekuja katika nchi ambapo hakuwa na makazi yake, na hakuna wakazi wa kumkaribisha wala familia tegemezi, wala mahusiano ambayo ni sababu ya hili, kuwa shupavu zaidi kuliko mgeni huyu ambaye ni mpita njia anayepita njiani kuelekea katika nchi yake. Kwa sababu mgeni anaweza kuishi katika nchi ya kigeni na akawa mkazi ndani yake, tofauti na msafiri anayetaka kwenda nchini kwake, haja yake huwa ni kupumzika ili apate wepesi na sio kukaa, na kuwa na hamu ya kuwasili katika nchi yake kama vile msafiri hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mwisho wa safari yake, halikadhalika muumini katika ulimwengu huu hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mahali pazuri.

Akazifanyia kazi bin Omari nasaha hizi na alikuwa akisema: Ukiamka usisubiri jioni, na ukishinda mpaka jioni usisubiri asubuhi, na ihesabu nafsi yako kuwa katika wafu walioko makaburini, na kwakuwa umri haukosi moja katika ya mawili, afya na maradhi; fanya haraka siku za afya yako kwa kufanya ibada kwa ajili ya maradhi yako; na tumia fursa ya matendo mema katika wakati wa afya kabla maradhi hayajakuzuia, na faidika na uhai wako katika dunia, kusanya ndani yake yale yatakayokunufaisha baada ya kifo chako.

Mafunzo: Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia

Makundi : Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha · Kuzitakasa Nafsi. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56