Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni ka…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni ka…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa…

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: إنه سمع نبي الله صلى الله عليه وسلم يقول: «لَو أَنَّكُمْ تَتَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ، لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزُقُ الطَّيْرَ، تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا».

Maelezo ya hadith: Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa…

Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.

Mafunzo: Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Fadhila za matendo ya moyoni. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
سبحان الله Gloire à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56