Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani …
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake juu ya kinywa chake, kwani Shetani …
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake…
Maelezo ya hadith: Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake…
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kupiga mwayo pale alipofungua kinywa chake kwa sababu ya uvivu au kujaa na mfano wake; kuwa aweke mkono wake juu ya kinywa chake ili akifunge kwa mkono; na hii ni kwa sababu Shetani huingia ndani yake anapokiacha wazi, kuweka mkono kunakuwa ni kizuizi cha kumzuia kuingia.
Mafunzo: Atakapopiga mwayo mmoja wenu basi na ashike mkono wake…
- Atakapotaka mtu kupiga miayo anatakiwa auzuie kwa kadiri awezavyo, kwa kuuzuia mdomo wake, na aubakishe ukiwa umefungwa wala usifunguke, asipoweza kuubakisha mdomo wake ukiwa umefungwa basi aweke mkono wake juu ya mdomo wake, afunike kinywa chake kwa mkono wake.
- Kushikamana na adabu za kiislamu katika hali zote; kwa sababu ndio anwani ya ukamilifu na tabia njema.
- Kuchukua tahadhari ya kila mapitio ya Shetani kwa mwanadamu.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za kupiga Chafya na Miayo.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
الحمد لله
Louange à Allah