Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge ud…
Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge ud…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na achelew…
عن أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُبْسَطَ لَهُ فِي رِزْقِهِ، وَيُنْسَأَ لَهُ فِي أَثَرِهِ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ».
Maelezo ya hadith: Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na achelew…
Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kuwaunga ndugu wa karibu kwa kuwatembelea na takrima za mwili na mali na mengineyo, nakuwa kufanya hilo ni sababu ya kukunjuliwa riziki, na kupewa umri mrefu.
Mafunzo: Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na achelew…
- Ndugu wa karibu ni wale wa upande wa baba na mama, na kadiri anavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo anavyokuwa bora zaidi kwa kuungwa udugu.
- Malipo huendana na matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ihisani, naye pia Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.
- Kuunga udugu ni sababu ya kukunjuliwa riziki na kupanuliwa kwake, na ni sababu ya umri mrefu, hata kama kifo na riziki vina muda maalum isipokuwa hili linaweza kuwa ni baraka katika riziki na umri, akafanya mengi katika umri wake na yenye manufaa zaidi kuliko atakavyofanya mwingine, na wanasema wanachuoni; ziada katika riziki na umri ni zaida ya uhalisia. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Ubora na fadhila za matendo mema.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
سبحان الله وبحمده
Gloire et louange à Allah