Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka …

Islam > Sw > Hadith > Fiqhi elimu ya dua na dhikri mbali mbali > Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka …

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Ibn Majah na Ahmad

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutok…

Maelezo ya hadith: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutok…

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimfundisha Aisha radhi za Allah ziwe juu yake dua inayokusanya mambo mengi nayo ni maombi manne:

La kwanza: Dua inayokusanya kila aina ya kheri: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe kutoka katika kheri zote" kwa ujumla wake, "Za haraka" zilizo karibu kwa wakati wake, na "za baadaye" za mbali, "Nilizozijua" katika zile ulizonifundisha, "na zile nisizozijua" katika zile zinazokuwa katika elimu yako ewe Mtukufu, Na hapa kuna kuyakabidhi mambo yote kwa Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye habari na Mpole; basi Mwenyezi Mungu humchagulia muislamu kilicho bora kati ya hayo na kizuri, "Na ninajilinda" ninashikamana na ninaomba ulinzi "kwako wewe dhidi ya shari zote, zinazokuja haraka na zinazochelewa, ninazozijua na nisizozijua".

Dua ya pili: Nayo ni kinga kwa muislamu ili asichupe mipaka katika dua "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba" na ninakutaka unipe "Katika kheri alizokuomba mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, "na ninajilinda kwako" na ninajiegemeza na kushikamana "kwako kutokana na shari alizojikinga nazo mja wako na Nabii wako" rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni dua na ni ombi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ampe muombaji yale aliyomuomba na akayataka Nabii Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake, pasina kusema aina ya yale aliyoyaomba rehema na amani ziwe juu yake.

Dua ya tatu: Kuomba kuingia peponi na kujiweka mbali na moto, nalo ni ombi la kila muislamu na ndio lengo kuu la matendo yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba pepo" na kufauli kuipata "Na yale yanayotuweka karibu nayo miongoni mwa kauli na matendo" mema yenye kukuridhisha, "na ninajilinda kwako kutokana na moto" kiasi kwamba hakuna kukingwa na matendo machafu ila kwa upole wako, "na yale yenye kutuweka karibu nao miongoni mwa kauli na matendo" katika maasi yanayokukasirisha.

Dua ya nne: Kuomba kuridhika na kadari za Mwenyezi Mungu "na ninakuomba uyafanya maamuzi yako uliyoyapitisha yawe ni kheri" na kila jambo alilolihukumu Mwenyezi Mungu kwangu alifanye kuwa ni kheri kwangu, na ni katika dua za kuomba kuridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutok…

Makundi : Fiq'hi -Elimu- ya Dua na Dhikri mbali mbali. · Dua zilizopokelewa toka kwa mtume. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mer. 16 Joumada 1
الأربعاء 16 جمادى الأولى
أحدب متناقص Gibbeuse Décroissante Jour 17.1 / 29.5
Illumination 94%
Nouvelle lune dans 12 jours
الله أكبر Allah est le plus grand

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56