Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuw…
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuw…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Twabraniy
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya…
Maelezo ya hadith: Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya…
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu aina tatu za watu, wenye kustahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa adhabu tatu, endapo hawatotubia au kusamehewa adhabu: Ya kwanza: Hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa sababu ya ukali wa ghadhabu yake, bali atawapuuza, au atawasemesha maneno yasiyowafurahisha na yanayoonyesha hasira yake juu yao. Ya pili: Hatowatakasa wala hatowasifia wala hatowasafisha kutokana na madhambi. Ya tatu: Watakuwa na adhabu yenye kuumiza sana Akhera. Na watu wa aina hiyo ni: Aina ya kwanza: Mtu mzima na anajiingiza katika machafu ya zinaa. Ya pili: Fakiri asiyekuwa na mali lakini pamoja na hivyo ana kiburi kwa watu. Ya tatu: Anayekithirisha kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu katika kuuza na kununua, analidhalilisha jina la Mwenyezi Mungu, na analifanya kuwa ndio nyenzo ya kujipatia mali.
Mafunzo: Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya…
- Amesema Kadhi Iyadhi katika sababu ya adhabu hii kali: Nikuwa kila mmoja miongoni mwao alishikamana na maasi haya yaliyotajwa pamoja nakuwa yuko mbali nayo, na hapakuwa na haja ya kufanya hivyo, na udhaifu wa vishawishi vyake kwake; hata kama hakuna anayepewa udhuru wa kufanya dhambi, lakini kwa sababu hapakuwa na haja ya kutenda maasi haya yenye kukera, wala kishawishi kilichozoeleka, hii inafanana na ukaidi, na kudharau haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaamua kumuasi si kwamba ana haja ya kufanya hivyo.
- Zinaa na uongo na kiburi ni katika madhambi makubwa.
- Kiburi: Ni kukataa haki, na kuwadharau viumbe.
- Tahadhari ya kukithirisha kutumia kiapo katika kuuza na kununua, na himizo la kuheshimu kiapo, na kuheshimu majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mtukufu: "Na wala msifanye Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa kisingizio cha kuacha kufanya wema" [Baqara: 224].
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuyasema vibaya Maasi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
حسبنا الله ونعم الوكيل
Allah nous suffit, quel excellent protecteur