Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasay…
Islam > Sw > Hadith > Adabu za kisheria > Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasay…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata…
Maelezo ya hadith: Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata…
Anatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu; kwani muumini haapi ila kwa Mwenyezi Mungu, Na anaeleza kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Kwa mfano mtu akiapa kwa Lata na Uzza - masanamu mawili yaliyokuwa yakiabudiwa katika zama za kabla ya Uislamu - basi aseme ndani ya nafsi yake: Hapana apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ili ajiepushe na ushirikina na ili iwe ni fidia ya kiapo chake hicho.
Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayemwambia rafiki yake: Njoo tucheze kamari - ambayo ni watu wawili au zaidi watakaposhindana kwa sharti kuwa baina yao kuna pesa ambayo mshindi ataichukua, na kila mmoja wao lazima ima apate hasara au faida-; ni sunna atoe sadaka kwa kitu chochote kama kafara ya yale aliyoyahamasisha.
Mafunzo: Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata…
- Kiapo hakiwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake.
- Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu, ama kuapa kwa masanamu kama Lata au Uzza au kuapia amana, au kuapa kwa Mtume au kitu kingine chochote.
- Amesema Khattwabi: Kiapo kinakuwa kwa Muabudiwa Mtukufu, basi akiapa kwa Lata na mfano wa hayo anakuwa kawaiga makafiri, basi akaamrishwa kukirekebisha kwa neno la tauhidi.
- Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu si lazima atoe kafara ya kiapo chake, bali anatakiwa kutubia na kuomba msamaha, kwa sababu hilo ni kubwa mno kuliko kusamehewa na kisichokuwa toba.
- Kumeharamishwa kamari kwa aina zake zote na mitindo yake yote, ambayo ni kamari aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akaiambatanisha na pombe na masanamu.
- Ulazima wa kurudi na kuacha maasi wakati wa kuyafanya.
- Atakayefanya jambo baya anatakiwa afuatishe jambo jema; kwa sababu matendo mema huondoa maovu.
Makundi :
Adabu za kisheria.
· Adabu za mazungumzo na kunyamaza.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
· Matamshi yaliyokatazwa na maafa ya ulimi.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad