Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini…
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia hii ni kama msafiri aliyeshuka chini…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia h…
Maelezo ya hadith: Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia h…
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilala juu ya busati dogo lililoshonwa kutokana na baadhi ya mimea, akasimama ukiwa tayari mkeka umeathiri katika ngozi ya ubavu wake, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau tungelikuandalia godoro laini basi ingelikuwa bora kuliko kujilaza kwako juu ya mkeka mgumu, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sina mapenzi wala hamu ya dunia mpaka niwe na tamaa nayo, kwani mfano wangu mimi na kubakia katika dunia ni kama msafiri aliyejikinga kivulini kwa muda mfupi kisha akaondoka akakiacha.
Mafunzo: Nina haja gani mimi na dunia, kwani mimi katika dunia h…
- Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuipa nyongo na kuipuuza dunia.
- Hadithi haijamaanisha kuacha mambo ya lazima katika dunia, bali imemaanisha kuishughulikia zaidi kuliko akhera, kwani mtu kakaa chini ya kivuli cha mti na akafaidika nacho kwa ajili ya kufika anakokwenda, na wala hakubweteka hapo.
- Kuchukua mazingatio kwa hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba atakayeiga nyenendo zake ataongoka, na atafaulu katika dunia na akhera.
- Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao juu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na mapenzi yao kwake.
- Sheria ya kupiga mifano katika ufikishaji ujumbe na ufundishaji.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Kuyasema vibaya mapenzi ya kuipenda dunia.
· Kuzitakasa Nafsi.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah