Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, hu…
Islam > Sw > Hadith > Mambo yaliyo bora > Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, hu…
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote…
Maelezo ya hadith: Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote…
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kung'arisha na muonekano na uzuri katika dunia, na amfikishe Mwenyezi Mungu katika mng'ao wa peponi na neema zake na mng'ao wake katika Akhera; kwa yule atakayesikia hadithi yake akaihifadhi ili amfikishie mwingine, huenda aliyenukuliwa hadithi akawa mwerevu na muelewa na akawa na uwezo wa kuchambua hukumu kuliko hata aliyeinukuu hadithi, akawa wa kwanza anahifadhi vizuri, na wa pili akawa anauelewa na uchambuzi mzuri.
Mafunzo: Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote…
- Himizo la kuhifadhi mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuyafikisha kwa watu.
- Kumebainishwa fadhila za watu wa hadithi, na heshima ya kuitafuta kwake.
- Fadhila ya wanachuoni, ambao wanastahiki kuchambua na kuzielewa hadithi.
- Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, wao ndio waliosikia hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakatufikishia.
- Amesema Al-Munaawi: Amebainisha kuwa mpokezi wa hadithi kuwa na uelewa si katika sharti zake, bali sharti lake ni kuhifadhi, na kwa msomi kuelewa na kuzingatia.
- Amesema bin Uyaina: Hakuna yeyote anayetafuta hadithi isipokuwa kuna mng'ao katika uso wake kwa hadithi hii.
- Kuhifadhi kwa wasomi wa hadithi kuna aina mbili: Kuhifadhi kwa moyo na kifua, na kuhifadhi kwa kitabu na mwandiko, na aina zote mbili zinakusanywa na dua iliyoko katika hadithi.
- Ufahamu wa watu unatofautiana, huenda mfikishiwa akawa muelewa zaidi kuliko aliyesikia, na huenda aliyebeba maarifa ya sheria akawa si muelewa.
Makundi :
Mambo yaliyo bora.
· Adabu za kisheria.
· Ubora wa Elimu.
· Adabu za mjuzi na mwenye kujifunza.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
أستغفر الله
Je demande pardon à Allah