Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la k…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن عائشة رضي الله عنها قالت: سَأَلَ أُنَاسٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْكُهَّانِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسُوا بِشَيْءٍ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، فَإِنَّهُمْ يُحَدِّثُونَ أَحْيَانًا بِالشَّيْءِ يَكُونُ حَقًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تِلْكَ الْكَلِمَةُ مِنَ الْحَقِّ يَخْطَفُهَا الْجِنِّيُّ فَيَقُرُّهَا فِي أُذُنِ وَلِيِّهِ قَرَّ الدَّجَاجَةِ، فَيَخْلِطُونَ فِيهَا أَكْثَرَ مِنْ مِائَةِ كَذْبَةٍ».
Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wale wanaoeleza mambo yajayo yaliyofichikana, akasema: Msiwajali, na wala msiyachukue maneno yao, na wala msiyajali mambo yao.
Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao.
Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).
Makundi : Akida- Itikadi- · Kumuamini Allah mwenye nguvu aliye tukuka · Majina na Hukumu. · Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa Uungu wake. · (Mambo ya kale kabla ya uislamu)