Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: أقبَلَ رجل إلى نبي الله صلى الله عليه وسلم فقال: أُبَايِعُكَ على الهجرة والجهاد أَبْتَغِي الأجر من الله تعالى قال: «فَهَل لَكَ من وَالِدَيك أحد حيٌّ؟» قال: نعم، بل كلاهما، قال: «فتبتغي الأجر من الله تعالى؟» قال: نعم، قال: «فَارْجِع إلى وَالِدَيك، فَأَحْسِن صُحْبَتَهُمَا».
وفي رواية لهما: جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فاستأذنه في الجهاد، فقال: «أَحَيٌّ والداك؟»، قال: نعم، قال: «فَفِيهِمَا فجاهد».

Maelezo ya hadith: Hebu rudi kwa wazazi wako, na ukaishi nao vizuri

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimueleza kuhusu hamu yake na mapenzi yake ya jihadi na kuhama katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuwa huyu bwana kaacha nyuma yake wazazi wake wawili, na imekuja katika riwaya ya Abuudaudi kuwa "Walikuwa wakilia", wakihofia maisha yake, akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Je kuna yeyote kati ya wazazi wako wawili yuko hai?" Akasema: Ndiyo, bali wote wawili, akasema: "Na unatafuta malipo toka kwa Allah?" Akasema: Ndiyo, akasema: "Basi rudi kwao ukawachekeshe kama ulivyowaliza". Akamrudisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika lile ambalo ni bora katika haki zake, nalo ni kurudi kwa wazazi wawili na aishi nao vizuri, kwani hilo ni katika kupambana na nafsi katika kusimamia kuwahudumia na kuwaridhisha na kuwatii, kama ilivyokuja katika riwaya ya Bukhariy na Muslim: "Basi kwao wao wawili pigana jihadi". Na aliweka wazi katika hadithi nyingine kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili na kuwatii na kuwafanyia mazuri ni bora zaidi kuliko kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyokuja katika riwaya nyingine ya kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Anasema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamuuliza kuhusu amali bora, akasema: "Ni swala" Akasema: kisha nini?: Akasema: "Jihadi" akasema: Hakika mimi nina wazazi wawili, akasema: "Kuwafanyia kwako wema wazazi wawili ndiyo bora" ameitoa bin Hibbaani, Imeonyesha hadithi hii kuwa kuwafanyia wema wazazi wawili ndiyo bora kuliko Jihadi, isipokuwa kama itakuwa Jihadi ni faradhi ya lazima, basi hapo itatangulizwa juu ya kuwatii wao; kwasababu ya ulazima wake.

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Kuwatendea Wema wazazi wawili: · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
لا حول ولا قوة إلا بالله Pas de force ni de puissance sauf en Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56