Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia y…

Islam > Sw > Hadith > Mambo mazuri na adabu heshima > Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya dunia, Mwenyezi Mungu atamtatulia y…

Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 2 min de lecture

Maandishi ya hadith: Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya…

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيَا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ يَسَّرَ عَلَى مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَاللهُ فِي عَوْنِ الْعَبْدِ مَا كَانَ الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ، وَمَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْمًا سَهَّلَ اللهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ إِلَّا نَزَلَتْ عَلَيْهِمِ السَّكِينَةُ، وَغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وَحَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ، وَذَكَرَهُمُ اللهُ فِيمَنْ عِنْدَهُ، وَمَنْ بَطَّأَ بِهِ عَمَلُهُ لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ».

Maelezo ya hadith: Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya…

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa malipo ya muislamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni kulingana na yale anayoyatenda muislamu pamoja na waislamu wenzake; atakayetatua na akafariji na akaondoa, na ampa nafuu muumini ya dhiki na tabu miongoni mwa shida za dunia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa kumtatulia tatizo miongoni mwa matatizo ya siku ya Kiyama. Na atakayemfanyia wepesi mwenye hali ngumu na akamrahisishia na akamuondolea ugumu wake, basi naye Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi katika dunia na Akhera. Na atakayemsitiri muislamu, kama akiyaona kwake yale yasiyofaa kudhihirishwa katika mapungufu na kuteleza, basi naye Mwenyezi Mungu atamsitiri duniani na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anakuwa mwenye kumsaidia mja wake, pale ambapo mja anapokwenda mbio kumsaidia ndugu yake katika masilahi yake ya dunia na Akhera, na msaada unakuwa kwa kumuombea dua, au kwa mwili na mali na mengineyo. Na atakayekwenda kwa ajili kutafuta elimu ya kisheria, akikusudia kupata radhi za Mwenyezi Mugnu Mtukufu; Mwenyezi Mungu atamfanyia wepesi kwa elimu hiyo njia ya kuingia pepnoni. Na hawatojikusanya watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu, wakikisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu, na wakifundishana baina yao, isipokuwa huwateremkia utulivu na amani, na huwafunika na kuwaenea rehema ya Mwenyezi Mungu, na Malaika huwafunika, na Mwenyezi Mungu huwasifia kwa wale walio karibu kwake, na inatosha kuwa ni fahari kwa mja kutajwa na Mwenyezi Mungu kwa wale walioko juu. Na yatakayekuwa matendo yake ni pungufu, hayatomuunganisha na watu wenye vyeo kwa ajili ya matendo yao, anatakiwa asibweteke kwa utukufu wa nasaba na ubora wa baba zake, na akafanya uzembe katika amali.

Mafunzo: Atakayemtatulia muumini tatizo moja katika matatizo ya…

Makundi : Mambo yaliyo bora. · Ubora wa Elimu. · Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.5 / 29.5
Illumination 97%
Nouvelle lune dans 13 jours
أستغفر الله Je demande pardon à Allah

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56