Islam > Sw > Hadith > Fiqhi na misingi yake > Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema:…
SahihiMis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lectureعن عَبْد اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قال: «أّعْتَمَ النَبِيُّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِالعِشَاء، فَخَرَج عُمَر فقال: الصَّلاةَ يا رسول الله، رَقَد النِسَاءُ والصِّبيَان. فَخَرَجَ ورَأسُهُ يَقطُر يقول: لَولاَ أن أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي -أو على النَّاس- لَأَمَرتُهُم بهذه الصَّلاة هذه السَّاعَة».
Alichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.
Makundi : Fiq'hi- Ufahamu- wa Ibada mbalimbali. · Sala. · Historia ya Mtume. · Fiq'hi na misingi yake. · Mambo ya Mtume. · Masharti ya Swala. · Sifa za kitabia. · Huruma yake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: · Historia na Taarekh.