Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi

Islam > Sw > Hadith > Akida itikadi > Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi

Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Sahihi

Mis à jour le 26 octobre 2026

📖 1 min de lecture

Maandishi ya hadith: Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni,…

عَنْ ‌أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ افْتَقَدَ ثَابِتَ بْنَ قَيْسٍ، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنَا أَعْلَمُ لَكَ عِلْمَهُ، فَأَتَاهُ فَوَجَدَهُ جَالِسًا فِي بَيْتِهِ، مُنَكِّسًا رَأْسَهُ، فَقَالَ: مَا شَأْنُكَ؟ فَقَالَ شَرٌّ، كَانَ يَرْفَعُ صَوْتَهُ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ، وَهُوَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَأَتَى الرَّجُلُ فَأَخْبَرَهُ أَنَّهُ قَالَ كَذَا وَكَذَا، فَرَجَعَ الْمَرَّةَ الْآخِرَةَ بِبِشَارَةٍ عَظِيمَةٍ، فَقَالَ: «اذْهَبْ إِلَيْهِ فَقُلْ لَهُ: إِنَّكَ لَسْتَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، وَلَكِنْ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ».

Maelezo ya hadith: Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni,…

Alimkosa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake, akamuulizia, mtu mmoja akasema: Mimi naweza kukupatia habari zake, na sababu ya kukosekana kwake, akamwendea akamkuta akiwa na huzuni na kainamisha kichwa chake nyumbani kwake, akamuuliza: Umepatwa na nini? Thabiti akamueleza shari aliyonayo; kwa sababu yeye alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mwenyezi Mungu kamuonya mwenye kufanya hivyo kwa kubatilika matendo yake, na kwamba yeye ni katika watu wa motoni.

Yule bwana akarejea kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na akamueleza hilo, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha arudi kwa Thabiti na ampe habari njema, yakuwa yeye si miongoni mwa watu wa motoni bali ni katika watu wa peponi, na hii ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye sauti ya juu kimaumbile, nakuwa yeye ndiye alikuwa mzungumzaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na ni mzungumzaji wa Answari (Watu wa Madina).

Mafunzo: Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni,…

Makundi : Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao. · Akida- Itikadi- · Maswahaba .

بسم الله الرحمن الرحيم mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
بدر Pleine Lune Jour 16.6 / 29.5
Illumination 96%
Nouvelle lune dans 13 jours
اللهم صل على محمد Ô Allah prie sur Muhammad

إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا

Al-Ahzab 33:56