Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu haya…
Islam > Sw > Hadith > Fiqhi ufahamu kuhusu familia > Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayozungumzwa na nafsi zao, madamu haya…
Hadith imesimuliwa na: Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayo…
Maelezo ya hadith: Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayo…
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Muislamu haadhibiwi kwa mazungumzo ya shari ya nafsi yake kabla ya kuyafanyia kazi au kuyazungumza, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu ameondolea uzito na kusamehe, na hakuuandikia makosa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa yale yanayopatikana akilini na yakazunguka katika nafsi bila ya kutulizana nafsi katika hiyo; yakitulizana katika moyo wake, mfano kama kiburi na kujiona au unafiki, au akafanya kwa viungo vyake au akasema kwa ulimi wake basi hapa atahesabiwa.
Mafunzo: Hakika Mwenyezi Mungu amewafutia umma wangu yale yanayo…
- Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, ameyaacha na kuyasamehe mawazo na fikira zinazojitokeza katika nafsi, mtu huzungumza mwenyewe ndani ya moyo wake na kupita katika mawazo yake.
- Mtu atakapofikiria talaka, na ikapita akilini mwake, lakini akawa hajaitamka na wala hajaiandika, basi hiyo haizingatiwi kuwa ni talaka.
- Mazungumzo ya nafsi mtu hahesabiwi vyovyote vile yatakavyokuwa makubwa madam hayajakita ndani ya nafsi yake na akayafanyia kazi au kuyazungumza.
- Ukubwa wa cheo cha umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake kwa kufanywa maalum kwa kutokuadhibiwa kwa mazungumzo ya nafsi, kinyume na umma zilizokuwa kabla yetu.
Makundi :
Fiq'hi- ufahamu- kuhusu familia.
· Talaka.
· Fiq'hi na misingi yake.
· Matamko ya Talaka.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
اللهم صل على محمد
Ô Allah prie sur Muhammad