Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu
Islam > Sw > Hadith > Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha > Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu
Hadith imesimuliwa na: Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Mis à jour le 26 octobre 2026
📖 1 min de lecture
Maandishi ya hadith: Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania…
Maelezo ya hadith: Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania…
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza muislamu kuwa asife isipokuwa katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu kwa kuwa na matarajio makubwa ya kheri wakati wa kufikwa na mauti kuwa Mwenyezi Mungu atamhurumia na kumsamehe, kwa sababu hofu hutakiwa kwa ajili ya kufanya vizuri katika matendo, na katika hali hiyo si hali ya kufanya amali yoyote, kinachotakiwa hapo nikuwa na matumaini makubwa.
Mafunzo: Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania…
- Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuuelekeza umma wake, na huruma yake kubwa kwao katika hali zake zote; hata katika maradhi ya kifo chake unaunasihi umma wake na anauelekeza katika njia za kuokoka.
- Amesema Attwaibi: Fanyeni matendo yenu kuwa mazuri hivi sasa ili dhana yenu iwe nzuri kwa Mwenyezi Mungu wakati wa kifo, kwani yatakayekuwa mabaya matendo yake kabla ya kifo chake atakuwa na dhana mbaya wakati wa kufa kwake.
- Hali kamili ya mja nikuwa kati ya matumaini na hofu, na mapenzi makubwa; mapenzi ndio kipando, na matumaini ndio gurudumu, na hofu ndio mwendo, na Mwenyezi Mungu ndiye mfikishaji kwa neema zake na karama zake.
- Inalazimu kwa atakayekuwa karibu na aliyefikwa na mauti azidishe kwake kumpa matumaini na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, katika hadithi hii Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameyasema haya kabla ya kufa kwake kwa siku tatu.
Makundi :
Tungo zenye kulainisha moyo na mawaidha
· Matendo ya moyoni.
· Mambo mazuri na Adabu- Heshima.
بسم الله الرحمن الرحيم
mar. 15 Joumada 1
الثلاثاء 15 جمادى الأولى
لا حول ولا قوة إلا بالله
Pas de force ni de puissance sauf en Allah